Pata taarifa kuu
UGANDA-SOKA

Uganda wajiweka sawa kupepetana na Tanzania

Timu ya taifa ya soka ya Uganda yenye vijana wasiozidi miaka 17, inamalizia mazoezi kabla ya kwenda nchini Tanzania, kushiriki katikla fainali ya bara Afrika itakayoanza mwishoni mwa wiki hii jijini Dar es Salaam.

Mashabiki wa Taifa Stars wakati ilipokua ikifuana na Cote d'Ivoire  June 16 mwaka 2013.
Mashabiki wa Taifa Stars wakati ilipokua ikifuana na Cote d'Ivoire June 16 mwaka 2013. YouTube
Matangazo ya kibiashara

Kocha wa viungo Derrick Owusu Osei chini ya usimamizi wa kocha mkuu Paa Samuel Kwesi kutoka Ghana wamekuwa wakijiandaa kwa michuano hiyo ambayo Uganda itashiriki kwa mara ya kwanza.

The Cubs kama wanavyofahamika, wamepangwa katika kundi moja na wenyeji Tanzania, Nigeria na Angola.

Mechi ya kwanza itakuwa ni kati ya Angola siku ya Jumapili.

Mataifa mengine yanayoshiriki katika michuano hiyo ambayo yamepangwa ni pamoja na Guinea, Cameroon, Morocco na Senegal.

Washindi wawili wa kila kundi, watafuzu katika hatua ya nusu fainali na hatimaye kombe la dunia nchini Brazil baadaye mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.