rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

AFCON DRC Liberia

Imechapishwa • Imehaririwa

DRC yaishinda Liberia kufuzu fainali ya AFCON kwa mara ya 19

media
Rais wa DRC Felix Tshisekedi akisherehekea bao katika mechi muhimu dhidi ya Liberia, Machi 24 2019 twitter.com/fecofa

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imefuzu katika fainali ya mchezo wa soka kuwania ubingwa wa mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Liberia katika uwanja wa Tata Raphael, jijini Kinshasa.


Mechi hiyo ilikuwa ni muhimu sana kwa Leopard kupata ushindi lakini bao la Cedric Bakamu lilitosha kuwafikisha vijana wa Florient Ibenge katika fainali yao ya 19.

Pamoja na DRC, Zimbabwe nayo imefuzu baada ya kuilaza Congo Brazaville mabao 2-0 katika uwanja wa taifa jijini Harare.

Brave Warriors walipata ushindi huo kupitia, wachezaji wake Khama Billiat katika dakika ya 20 kipindi cha kwanza, huku Knowledge Musona katika dakika ya 36.

Zimbabwe sasa imefuzu mara tatu katika histori ya AFCON mara ya kwanza ikiwa ni mwaka 2004, 2006, 2017 na sasa 2019.

Imemaliza kundi la G kwa alama 11, mbele ya DRC ambayo imemaliza ya pili kwa alama 9.

Liberia ambayo ilienda Kinshasa na matumaini makubwa ya kufuzu, imemaliza katika nafasi ya tatu kwa alama 7 huku Congo Brazaville ikiwa ya mwisho kwa alama tano.