rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Ulaya UEFA Paris Saint-Germain Manchester United

Imechapishwa • Imehaririwa

PSG waangukia pua kwa kufungwa na Man United 3-1

media
Mshambuliaji wa PSG Kylian Mbappé. Reuters/John Sibley

Paris Saint-Germain wameondolewa na Manchester United katika mzunguko wa 16 wa Kombe la Ulaya la ligi ya Mabingwa), Machi 6, 2019. PSG wamefungwa 3-1 wakiwa nyumbani licha ya kushinda 2-0 katika mechi ya awali


Mchezaji Marcus Rashfors, alifunga penalti katika kipindi cha majeruhi na kuisaidia Manchester United kufuzu katika hatua ya robo fainali, kuwania taji la klabu bingwa barani Ulaya baada ya kuishinda Paris Saint Germain jijini Paris Jumatano usiku kwa mabao 3-1 katika mechi ya marudiano.

Mechi ya kwanza, nchini Uingereza, Manchester United walipoteza nyumbani mabao 2-0 na ushindi wa jana Jumatano uliwashangaza wengi, na imefuzu sababu ya bao la ugenini baada ya timu zote kutoka sare ya mabao 3-3.

Manchester united sasa inaugana na klabu nyingine, ya uingereza Tottenham Hotspur FC katika hatua ya robo fainali.

Porto ya Ureno, nayo ikiwa nyumbani, iliishinda Roma ya Italia mabao 3-1 na kulipiza kisasi, ya kufungwa mabao 2-1 katika mechi ya kwanza, na mechi hiyo ilimalizika kwa jumla ya mabao 4-3.

Mechi nne, zinazosalia zitachezwa wiki ijayo, Liverpool dhidi ya Bayern Munich, Lyon dhidi ya Barcelona, Atletico Madrid nayo watapambana na Juventus, huku Schalke 04 wakichuana na Manchster City.

Mechi hizi zitachezwa tarehe 12 na 13 mwezi huu.