rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Paris Saint-Germain Manchester United UEFA

Imechapishwa • Imehaririwa

Ligi ya Mabingwa: PSG yaiburuza Manchester United kwa 2-0

media
Mchezaji wa PSG Angel Di Maria (kushoto) na nyota wa Manchester United Paul Pogba. REUTERS/Phil Noble

Paris Saint-Germain wamepata ushindi mkubwa wa mabao 2-0 dhidi ya Manchester United katika mzungukoa wa nne wa Kombe la Ulaya la klabu (Ligi ya mabingwa) Jumanne Februari 12, 2019.


Hii ni mara ya kwanza klabu ya Ufaransa kupata ushindi kwenye uwanja wa klabu ya Uingereza, katika michuano ya Ligi ya Mabingwa.

Paris Saint-Germain (PSG) licha ya kuwakosa wachezaji wake nyota, Neymar, na Edinson Cavani, ambao walijeruhiwa, walipata ushindi wa kutosha dhidi ya wenyeji wao Manchester United.

Paul Pogba, mchezaji nyota wa Manchester United alitupwa nje dakika ya mwisho ya muda wa ziada alipolishwa kadi ya njano mara ya pili katika hatua ambayo itamkosesha mechi ya marudio.

Mabao ya mabingwa wa Ufaransa (PSG) yaliwekwa kimyani na Presnel Kimpembe pamoja na Kylian Mbappe.

Manchester United wanahitaji miujiza watakapokutana tena na miamba hao wa Ufaransa mjini Paris Machi 6 ili wafuzu kuingia robo fainali.