Pata taarifa kuu
SENEGAL-CAF-FIFA-SOKA

Young Lions of Teranga yafuzu katika fainali ya Kombe la Dunia

Timu ya taifa ya Senegal yenye vijana wasiozidi miaka 20, imekuwa ya kwanza kufuzu katika fainali ya Kombe la Dunia itakapigwa mwezi Mei nchini Poland.

Young Lions of Teranga yafuzu katika nusu fainali ya AFCON na katika Kombe la Dunia 2019 Poland.
Young Lions of Teranga yafuzu katika nusu fainali ya AFCON na katika Kombe la Dunia 2019 Poland. Senegal Footbal/twitter.com
Matangazo ya kibiashara

Hii imekuja baada ya Young Lions of Teranga kuishinda Ghana mabao 2-0 katika mechi ya pili, kuwania ubingwa wa Afrika, mashindano yanayoendelea nchini Niger.

Senegal wanaongoza kundi la B kwa alama sita, baada ya kucheza mechi ya kwanza dhidi ya Mali pia kwa mabao 2-0.

Mechi ya mwisho, Senegal itavaana na Burkina Faso siku ya Jumamosi.

Nigeria nayo inaendelea kuongoza kundi A kwa alama nne, baada ya kutofungana na Afrika Kusini katika mechi yake ya pili.

Wenyeji Niger na Afrika Kusini zina alama mbili, huku Burundi ikiwa na alama moja baada ya sare ya mabao 3-3 na Niger.

Michuano ya makundi inamalizika siku ya ijumaa, Niger itachuana na Nigeria huku Afrika Kusini ikimenyana na Burundi.

Timu tatu zinasubiriwa kufuzu katika michuano ya kombe la dunia baada ya michuano ya mwishoni mwa wiki hii.

Mataifa mengine yaliyofuzu kwingineko duniani ni pamoja na:-

Barani Asia: Japan, Korea , Qatar na Saudi Arabia

Bara la Amerika, Concacaf: Honduras, Mexico, Panama na Marekani.

Eneo la Visiwa na Bahari: New Zealand and Tahiti

Barani Ulaya: Ufaransa, Italia, Norway, Ureno na Ukraine 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.