Pata taarifa kuu
UINGEREZA-MANCHESTER-UNITED-SOKA

Manchester United wamtimua meneja wao Jose Mourinho

Klabu ya Manchester United imemtimua meneja wao Jose Mourinho baada ya kushindwa kufanya vizuri ilipokua ikitimua vumbi na Liverpool siku ya Jumapili.

Kocha wa Manchester United José Mourinho akitoa maagizo kwa Mfaransa Paul Pogba.
Kocha wa Manchester United José Mourinho akitoa maagizo kwa Mfaransa Paul Pogba. Reuters/Andrew Couldridge
Matangazo ya kibiashara

Kwa sasa Manchester United inaendelea na mchakato wa kumtafuta meneja mpya wa kudumu. Hata hivyo inatarajia kumteua hivi karibuni meneja wa muda atakayekaimu kwenye nafasi hiyo hadi mwisho wa msimu.

Jose Mourinho amekuwa Old Trafford kwa miaka miwili na nusu baada ya kuchukua mikoba kutoka kwa Louis van Gaal, raia wa Uholanzi, mwezi Mei 2016.

Mourinho alikuwa katika mzozano na mchezaji wake Paul Pogba ambaye amekuwa hachezeshwi tena katika kikosi cha kuanza mechi.

Paul Pogba ameonekana akikaribisha uamuzi huo wa Manchester United.

Paul Pogba alinunuliwa kwa bei iliyovunja rekodi ya klabu hiyo ya euro milioni 89.

Dsiku ya Jumapili Manchester United walichapwa na Liverpool uwanjani Anfield, mechi ambayo Pogba hakuchezeshwa.

Katika taarifa yake, Manchester United wamesema watamteua meneja mpya wa muda.

Kufutwa kwa Mourinho kunaendeleza historia yake ya kutomaliza misimu mitatu mfululizo katika klabu moja.

Majina ya Zinedine Zidane aliyekuwa meneja wa Real Madrid, meneja wa Atletico Madrid Diego Simeone na meneja wa sasa wa Tottenham Hotspur Mauricio Pochettino na meneja wa zamani wa Chelsea Antonio Conte wanazungumziwa kuchukuwa nafasi ya Jose Mourinho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.