rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Kenya Colombia Riadha

Imechapishwa • Imehaririwa

Kipchoge na Ibarguen washinda tuzo ya wanariadha bora wa mwaka 2018

media
Bingwa wa dunia wa mbio za Marathon Eliud Kipchoge baada ya kutuzwa na Umoja wa Mataifa jijini Nairobi REUTERS/Fabrizio Bensch

Bingwa wa dunia wa mbio za Marathon katika mchezo wa Riadha Mkenya Eliud Kipchoge na Mcolombia, Caterine Ibarguen anayeshiriki mashindano ya kuruka, ndio wanariadha bora wa mwaka 2018.


Kipchoge ameshinda tuzo hii baada ya mwezi Septemba kuvunja rekodi ya mbio za Marathon huko Berlin, nchini Ujerumani kwa muda wa saa mbili dakika moja na sekunde 39.

Mwanariadha huyo wa Kenya mwenye umri wa miaka 34, anatajwa kuwa mwanariadha bora wa mbio hizi ndefu katika miaka ya hivi karibuni.

Kati ya mashindano 11 ya Marathon aliyoshiriki, ameshinda 10 na kushinda mara tatu jijini London na Berlin bila kusahau wakati wa michezo ya Olimpiki mwaka 2016 nchini Brazil.