rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Timu ya Taifa ya Uholanzi Manchester United Arsenal FC Uturuki

Imechapishwa • Imehaririwa

Robin Van Persie atangaza kutundika daruga mwishoni mwa msimu

media
Robin Van Persie enzi hizo akiitumikia Manchester united ya Uingereza Sky Sports

Mshambuliaji wa zamani wa Kimataifa wa Uholanzi Robin Van Persei ametangaza kuwa atastaafu kucheza soka mwishoni mwa msimu huu.


Nyota huyo amewahi kuzichezea klabu za Fayernood ya Uholanzi, Arsenal na Manchester United za Uingereza, Fernebace ya Uturuki kabla ya kurejea nyumbani kwao kuichezea tena Fayernood.

Akiwa nchini Uingereza alishinda taji la FA akiwa na Arsenal na pia alishinda taji la Ligi Kuu akiwa na klabu ya Manchester united mwaka 2012.

Van Persie mwenye umri wa miaka 35 ameichezea Timu ya Taifa ya Uholanzi mara 102 na kufunga jumla ya mabao 50 na ameshiriki fainali kadhaa za Kombe la dunia zikiwemo za mwaka 2010 nchini Afrika Kusini na 2014 nchini Brazil.

Alipoulizwa na wanahabari Van Persie alisema “Lini nitastaafu, inawezekana mwishoni mwa msimu, nimekuwa kwenye mpira kwa miaka 18, nimekuwa sehemu ya soka”