Pata taarifa kuu
RIADHA-TANZANIA-KENYA-JUMUIYA YA MADOLA

Wanariadha wanane kuiwakilisha Tanzania, mashindano ya Jumuiya ya Madola

Tanzania itawakilishwa na wanariadha wanane katika mashindano ya riadha ya nusu marathoni yanayotazamiwa kufanyika Oktoba saba katika Mji wa Cardiff nchini Uingereza.

Mwanariadha Fabian Nelson akiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Simon Sirro baada ya kupandishwa cheo.
Mwanariadha Fabian Nelson akiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Simon Sirro baada ya kupandishwa cheo. Jeshi la Polisi Tanzania
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa katiobu mkuu wa Shirikisho la mvchezo wa riadha Tanzania (RT), Wilhelm Gidabudai mashindano hayo ya nusu marathoni ni ya kwanza kuandaliwa na Jumuiya ya Madola.

Baadhi ya wanariadha watakaoiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo yanayoandaliwa kwa mara ya kwanza ya nusu marathoni yaani kilometa 21.

“Ni mashindano ambayo nchi inawakilishwa moja kwa moja, ni sawa na mashindano ya jumuiya ya madola yaliyoandaliwa nchini Australia,” Gidabudai ameiambia Idhaa ya Kiswahili ya Radio France.

Baadhi ya wanariadha watakaoiwakilisha Tanzania ni Fabiano Nelson, Sara Ramadhan, Fainuna Abdi na Pascali Mombo.

Hata hivyo Tanzani, itakabiliwa na kibarua pevu kuwania medali katika mashindano hayo, kutokana na uwepo wa wanariadha kutoka mataifa ya Kenya na Afrika Kusini ambao wamekuwa wakifanya vizuri kwenye mashindano mbalimbali ya kimataifa.

Sikiliza mahojiano baina ya Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania, RT na mwandishi wa RFI, Fredrick Nwaka kupitia kiunganishi hapo juu.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.