Pata taarifa kuu
UFARANSA-SOKA-KOMBE LA DUNIA

Kombe la Dunia 2018: Les Bleus washerehekea ushindi wa kihistoria

Kuanzia saa moja usiku jana Jumapili mpaka usiku wa manane, wananchi wa Ufaransa kutoka ndani na nje ya nchi wamekua wakiendelea kusherehekea ushindi wa timu yao ya taifa, Les Bleus, dhidi ya Croatia.

Umati mkubwa wa watu ulivamia mtaa wa Champs-Elysées kwa furaha ya ushindi wa timu ya taifa ya Ufaransa, Paris, Julai 15, 2018. .
Umati mkubwa wa watu ulivamia mtaa wa Champs-Elysées kwa furaha ya ushindi wa timu ya taifa ya Ufaransa, Paris, Julai 15, 2018. . REUTERS/Charles Platiau
Matangazo ya kibiashara

Kwa mara ya pili katika historia yake, timu ya taifa ya Ufaransa wamekua mabingwa wa Kombe la Dunia mwaka huu baada ya kuiadhibu Croatia kwa mabao 4-2. Mashambiki kutoka maeneo mbalimbali ya nchi yalikua wakishrehekea ushindi huo kwenye mtaa wa Champs-Elysées, eneo la kihistoria mjini Paris.

Timu ya Taifa ya Ufaransa Les Blue imetwaa ubingwa wa fainali za kombe la dunia baada ya kusihinda Croatia mabao 4-2.

Mabao ya Ufaransa yamefungwa na Paul Pogba, Kylian Mbappe, Antoine Griezman na bao la kujifunga mshambuliaji wa Croatia, Mario Mandzukic.

Mabao ya Croatia yamefungwa na Mario Mandzukic na Ivan Perisic.

Kwa ushindi huo, Ufaransa inashinda taji la pili katika historia ya Kombe la dunia, wakati Kocha Didier Deschamps pia anaweka rekodi ya kushinda taji hilo mara mbili.

Mara ya kwanza Ufaransa ilishinda taji hilo mwaka 1998, fainali zilizofanyika nchini Ufaransa, Deschamps alikuwa nahodha wa kikosi cha Ufaransa kilichoshinda taji hilo.

Hili ni mara ya kwanza kwa Croatia, taifa lenye idadi ya watu milioni 4 kufika fainali ya michuano hiyo, mara ya mwisho walifika nusu fainali mwaka 1998, fainali zilizoandaliwa na Ufaransa.

Kabla ya kufika fainali Ufaransa iliishinda Ubelgiji katika mchezo wa nusu fainali kwa bao 1-0 lililofungwa na Samuel Umtiti, Croatia wao waliwafunga Uingereza kwa mabao 2-1.

Hizi huenda zikawa fainali za mwisho za Kombe la dunia kwa wachezaji Luka Modric, Olivier Giroud ambao wana umri wa miaka zaidi ya 30.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.