rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Yanga SC

Imechapishwa • Imehaririwa

Yanga yawarejesha kundini Mrisho Ngassa na Deus Kaseke

media
Deus Kaseke (kulia) na Mrisho Ngassa (kushoto) wakitambulishwa na mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Yanga, Hussein Nyika www.yangasc.co.tz

Klabu ya Yanga ya Tanzania imewasajili wachezaji Deus Kaseke na Mrisho Ngassa kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.


Wachezaji hao wametambulishwa leo katika makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo Jangwani na Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Yanga Hussein Nyika.

Wachezaji wote waliwahi kuitumikia Yanga kwa misimu tofauti. Deus Kaseke anajiunga na Yanga akitokea Singida United na Kaseke anatokea Singida United.

Wachezaji wengine waliosajiliwa na Yanga ni Mohammed Issa kutoka Mtibwa Sugar na Jafar Mohammed kutoka Majimaji ya Songea.

Yanga ni wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Afrika ambapo wanashiriki hatua ya makundi ya taji la shirikisho.