Pata taarifa kuu
KOMBE LA DUNIA-UFARANSA-CROATIA

Croatia yafukuzia rekodi Kombe la dunia

Croatia inachuana na Ufaransa katika fainali ya Kombe la dunia katika Uwanja wa Luzhniki Mjini Moscow ikilenga kushinda taji la kwanza katika soka la kimataifa. 

Wachezaji wa croatia wakishangilia katika mojawapo ya michezo ya fainali za Kombe la dunia
Wachezaji wa croatia wakishangilia katika mojawapo ya michezo ya fainali za Kombe la dunia REUTERS/Henry Romero
Matangazo ya kibiashara

Wapinzani wao,Ufaransa wanacheza fainali ya tatu ya kombe la duinia wakiwa wameshinda mara moja na kupoteza fainali moja.

Croatia haijawahi kushinda taji hilo lakini inaundwa na wachezaji mahiri wakiwemo Luka Modric na Ivan Rakitic ambao wamekuwa injini katika idara ya kiungo.

"Ndoto, Ndoto, Ndoto! Croatia inacheza fainali ya kombe la dunia," limearifu gazeti la michezo la kila siku nchini Croatia, Sportske Novosti.

Rekodi nyingine iliyowekwa hii leo ni Croatia kuwa taifa la kwanza lenye idadi ndogo ya watu kufuzu kucheza fainali ya Kombe la dunia, inakisiwa kuwa na watu milioni 4.17

Je, watashinda taji hili, ni suala la kusubiri hivi leo kuanzia saa 12 kwa saa za Afrika Mashariki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.