rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Kombe la Dunia Urusi 2018 Urusi Ubelgiji Uingereza

Imechapishwa • Imehaririwa

Uingereza na Ubelgiji kutafuta ushindi wa kujiliwaza

media
Mechi iliyopita kati ya Uingereza na Croatia 路透社

Ubelgiji itamenyana na Uingereza katika mchuano muhimu wa kumtafuta mshindi wa tatu katika michuano ya kombe la dunia, inayomalizika siku ya Jumapili jijini Moscow nchini Urusi.


Mbali na kuwa mchuano muhimu wa kumtafuta mshindi wa tatu, ni mechi ambayo pia timu zote mbili zitatafuta kujiliwaza baada ya machungu ya kuondolewa katika hatua ya nusu fainali.

Uingereza ilipoteza mchuano wake dhidi ya Croatia baada ya kufungwa mabao 2-1 katika muda wa ziada huku Ufaransa ikiishinda Ubelgiji bao 1-0.

Mwaka 1954, wakati mataifa haya yalipokutana katika michuano hii ya kombe la dunia, yalitoka sare ya mabao 4-4 katika hatua ya makundi.

Mwaka 1990, Uingereza iliishinda Ubelgiji bao 1-0 katika hatua ya mwondoano wakati fainali hizi zilipochezwa nchini Italia.

Wachezaji wa kuangaliwa sana katika mechi hii ni nahodha na mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane kwa upande wa Uingereza na mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku.

Hawa ni wachezaji wanaotarajiwa kuanza mechi hiyo:

Ubelgiji: Mignolet, Vermaelen, Boyata, Kompany, Dendoncker, Dembele, Fellaini, Chadli, Januzaj, Mertens, Batshuayi

Uingereza: Butland, Cahill, Stones, Jones, Alexander-Arnold, Rose, Dier, Loftus-Cheek, Delph, Rashford, Vardy