rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Chelsea Uingereza Antonio Conte

Imechapishwa • Imehaririwa

Chelsea yamfuta kazi Antonio Conte

media
Kocha wa zamani wa Chelsea Antonio Conte REUTERS

Klabu ya soka ya Chelsea nchini Uingereza imemfuta kazi kocha wake Antonio Conte.


Conte mwenye umri wa miaka 48, raia wa Italia anaondoka katika klabu hiyo baada ya kuifunza kwa miaka miwili.

Kocha huyo amefutwa kazi, mwaka mmoja kabla ya mkataba wake kumalizika.

Mwezi Mei, aliisaidia Chelsea kunyakua taji la Shirikisho la soka nchini humo FA.

Msimu wa soka wa mwaka 2016/17, aliiwezesha Chelsea kumaliza katika nafasi ya tano matokeo ambayo yameikosesha klabu hiyo kushiriki katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.

Ripoti zinasema kuwa kocha wa zamani wa Napoli, Maurizio Sarri anatarajiwa kuwa kocha mpya wa Chelsea.