rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Simba SC Kombe la Kagame CECAFA

Imechapishwa • Imehaririwa

Nusu fainali ya Kagame Cup kuchezwa kesho

media
Simba imeshinda mataji sita ya Kombe la Kagame tangu mashindano hayo yalipoanza mwaka 1974 Goal.com

Michuano ya Kombe la Kagame inaendelea kesho kwa mechi za nusu fainali ambapo Simba itachuana na JKU ya Zanzibar.


Mchezo mwingine utakuwa baina ya Gor Mahia na Azam.

Simba iliishinda AS Sports ya Djibout katika robofainali na JKU iliishinda Singida United kwa mikwju ya penati 4-3 katika robo fainali baada ya kutoka suluhu kwa dakika 120.

Mabingwa wa Kenya Gor Mahia waliiondoa Vipers ya Uganda kwa mabao 2-1 nayo Azam jana iliilaza Rayon Sports kwa mabao 4-2.

Mashindano hayo yanayofanyika kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2015 yatafikia tamati Julai 13 kwa mchezo wa fainali na ule wa kusaka mshindi wa tatu.