rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Kombe la Dunia Urusi 2018 Timu ya Taifa ya Ubelgiji Timu ya Taifa ya Ufaransa

Imechapishwa • Imehaririwa

Nusu fainali ya kwanza kombe la dunia, kuchezwa kesho

media
Wachezaji wa Ufaransa wakishangilia baada ya kuishinda Uruguay katika mchezo wa robo fainali REUTERS/Grigory Duko

Nusu fainali ya kwanza ya kombe la dunia inachezwa kesho baina ya Ubelgiji na Ufaransa.


Mchezo huo ni muhimu kwa makocha wote, Roberto Martinez wa Ubelgiji na Didier Deschamps wa Ufaransa.

Deschamps anataka kuweka rekodi ya kushinda taji hili akiwa meneja baada ya kuiongoza Ufaransa kushinda taji hilo mwaka 1998 akiwa nahodha wa kikosi cha dhahabu.

Martinez kwa upande wake anaongoza kikosi cha dhahabau kinachotajwa kuwa na wachezaji wengi nyota katika historia ya soka la Ubelgiji.

Ebelgiji iliwaondoa Brazil katika hatua ya robo faainali kwa mabao 2-1 wakati Ufaransa iliinyuka Uruguay kwa mabao 2-0.