rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Timu ya Taifa ya Uhispania Real Madrid FC

Imechapishwa • Imehaririwa

Kocha wa Hispania ajiuzulu baada yaa kuhudumu kwa siku 25

media
Aliyekuwa Kocha wa timu ya Taifa ya Hispania Fernando Hierro REUTERS/Stringer

Kocha Fernando Hierro aliyeiongoza Hispania katika fainali za Kombe la dunia amejiuzulu katika nafasi yake.


Aidha ameachia ngazi kama mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo.

Hierro, mchezaji wa zamani wa Real Madrid na Timu ya Taifa ya Hispania alitangazwa meneja mpya siku mbili kabala ya kuanza kwa fainali za Kombe la dunia nchini Urusi baada ya kufutwa kazi kwa Julen Lopetegu ambaye alitangaza kuingia makubaliano yaa kuinoa Real Madrid baada ya fainali za kombe la dunia.

Licha ya kuongoza kundi B, Hispania, mabingwa wa mwaka 2010 Hispania ilifurushwa nje ya michuano hiyo na Urussi kwa changamoto ya mikwaju ya penati.