rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Kombe la Dunia Urusi 2018 Timu ya Taifa ya Croatia Timu ya Taifa ya Uingereza

Imechapishwa • Imehaririwa

Dalic: Croatia inaweza kumzuia Harry Kane

media
Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya England, Harry Kane REUTERS/Carlos Barria

Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Croatia Zlatko Dalic amesema kikosi chake kinaweza kumzuia Harry Kane kama ilivyofanikiwa kumzuia Lionel Messi.


Croatia itachuana na England siku ya Jumatano Mjini Moscow katika mchezo wa pili wa nusu fainali ya Kombe la dunia utakaoamua timu ipi itafuzu kucheza fainali Julai 15.

Licha ya kusema timu yake inaweza kumzuia Kane, Dalic amewataja Raheem Sterling na Kane kuwa ni wachezaji wa kuchungwa katika mchezo huo wa Jumatano.

“Tuna imani kulingana na uwezo tulionao, hatuwahofii England, Si rahisi kumzuia Harry Kane lakini tuna mabeki bora duniani,”amesema Dalic

Croatia iliyojinyakulia uhuru mwaka 1991 kwa mara ya pili inafuzu kucheza nusu fainali ya Kombe la dunia, mara ya mwisho ilikuwa mwaka 1998 nchini Ufaransa ambapo ilimaliza ya tatu.