rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Arsenal FC

Imechapishwa • Imehaririwa

Arsenal inakaribia kuwasajili Lucas Torreira na Matteo Guendouzi

media
Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Uruguay Lucas Torreira ambaye anatarajiwa kusajiliwa na Arsenal The Sun

Klabu ya Arsenal ya England inaelekea kukamilisha usajili wa wachezaji Lucas Torreira na Matteo Guendouzi.


Ripoti zilizochapishwa na kituo cha Sky Sports zinaarifu kuwa Torreira yu njia kuelekea London kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya na usajili wake unatajwa kugharimu Euro milioni 26.

Torreira anayetokea Sampdoria ya Italia, alikuwemo kwenye kikosi cha Uruguay kilichoshiriki fainali za Kombe la dunia na kuondolewa katika hatua ya robo fainali.

Aidha usajili wa Matteo Guendouzi, mchezaji wa timu ya vijana ya Ufaransa, kutoka Lorient ya Ufaransa unatajwa kugharimu Euro milioni nane.

Kocha Unai Emery anaimarisha kikosi chake tangu alipochukua mikoba ya kuinoa Arsenal baada ya kujiuzulu kwa Arsene Wenger.