rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Kombe la Dunia Urusi 2018 Timu ya Taifa ya Ufaransa Timu ya Taifa ya Ubelgiji

Imechapishwa • Imehaririwa

Ufaransa, Ubelgiji ni kufa au kupona Kombe la dunia

media
Kikosi cha Ufaransa kikisherehekea baada ya ushindi dhidi ya Uruguay kwa mabao 2-0, Julai 6 2018 www.fifa.com

Timu za Taifa za Ufaransa 'Le Blues' na Ubelgiji zinaendelea na maandalizi kabambe kabla ya kuchuana jumanne, ukiwa ni mchezo wa kwanza wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la dunia.


Ufaransa ilifika hatua hiyo baada ya kuishinda Uruguay kwa mabao 2-0 wakati Ubelgiji iliiangusha Brazil kwa mabao 2-1.

Ufaransa itategemea zaidi wachezaji Antoine Griezman na Kylian Mbappe wakati Ubelgiji inayoundwa na nyota mbalimbali itategemea kiungo wa chelsea Eden Hazard na Romelu Lukaku.

Mshindi baina ya Ufaransa na Ubelgiji atachuana na mshindi baina ya England na Croatia katika fainali itakayochezwa Julai 15.