rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Mahakama ya China yazuia mauzo ya iPhone kufuatia ombi la Qualcomm
  • Nadia Murad, mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel 2018, aomba "ulinzi wa kimataifa" kwa jamii ya Yazidi
  • Nchi itayoandaa michuano ya AFCON 2018 itajulikana Januari 9 kwa mujibu wa rais wa Shirikisho la Soka Afrika

Kombe la Dunia Urusi 2018 Uingereza Ufaransa Uruguay

Imechapishwa • Imehaririwa

Ufaransa, Ubelgiji zafuzu nusu fainali ya kombe la dunia

media
Kikosi cha Ufaransa kikisherehekea baada ya ushindi dhidi ya Uruguay kwa mabao 2-0, Julai 6 2018 www.fifa.com

Jumamosi ni siku ya pili ya mechi za robo fainali. Sweden watacheza na Uingereza katika uwanja wa Cosmos Arena, nchini Urusi katika mchuano muhimu wa kombe la dunia.


Baadaye saa tatu usiku, wenyeji wa Urusi itacheza na Croatia katika uwanja wa Olimpiki mjini Sochi.

Kabla ya kuthathmini mechi hizi za leo, jana kulikuwa na michuano miwili ya robo fainali,Ufaransa iliifunga Uruguay mabao 2-0.

Mabao ya Ufaransa yalifungwa na Raphael Varane katika dakika ya 40 huku Antoine Griezmann akitikisa nyavu dakika ya 61.

Mechi nyingine ya kukata na shoka, ilikuwa ni kati ya Brazil na Ubelgiji. Ubelgiji iliwashangaza mabingwa mara tano Brazil kwa mabao 2-1.

Fernandihno, alianza kwa kujifunga na kuipa nafasi Ubelgiji kuongoza kabla ya Kevin De Bruyne kufunga bap la pili katika dakika ya 31.

Brazil walijitahidi kutaka kusawazisha lakini mambo yalikuwa mazito, huku wakiambulia bao la kufuta machozi katika dakika ya 76 kupitia Renato Augusto.

Kwa maana hiyo Ubelgiji na Ufaransa watakutaa katika hatua ya nusu fainali siku ya Jumanne wiki ijayo mjini Saint Petersburg.

Uingereza vs Sweden:-

Mara ya kwanza kwa Uingereza kufikakatika hatua hii, mara ya mwisho ikiwa ni mwaka 2006.

Uingereza wanaamini kuwa, chini ya kocha Gareth Southgate amabye alikiteua kikosi chenye vijana chipukizi, kinaweza kushinda kombe hili.

Hii ni mara ya 25 kwa mataifa haya mawili kukutana na katika nyakati zote hizo, Uingereza wameshinda mara nane, huku Sweden wakishinda mara saba na kutoshana nguvu maara tisa.

Mara ya mwisho kwa mataifa haya mawili kukutana katika kombe la dunia, ilikuwa ni mwaka 2002 walipotoka sare ya bao 1-1 lakini pia mwaka 2006 na kutoshana nguvu pia kwa mabao 2-2.

Hii ni mechi ya tano ya robo fainali ya Sweden, na walifanikiwa kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali mwaka 1938, 1958 na 1994. Walipoteza mara moja tu mwaka 1934 dhidi ya Ujerumani.

Urusi vs Croatia

Timu zote zilifuzu katika hatua ya robo fainali, kupitia mikwaju ya penalti.

Mara ya mwisho kwa urisi kufika katika hatua hii ilikuwa ni mwaka1970 na wanakutana na Croatia ambayo hadi sasa haijafungwa katika michuano hii ya dunia, ila tu imefungwa mabao 2.

Katika mechi tatu walizokutana, Croation imeshinda zote mara ya mwishi ikiwa ni mwaka 2015, ilipoishinda mabao 3-1.

Kikosi:-Urusi: Igor Akinfeev; Mario Fernandes, Ilya Kutepov, Sergey Ignashevich, Fedor Kudryashov; Roman Zobnin, Daler Kuzyaev; Aleksandr Samedov, Aleksandr Golovin, Denis Cheryshev; Artem Dzyuba.

Croatia: Danijel Subasic; Sime Vrsaljko, Dejan Lovren, Domagoj Vida, Ivan Strinic; Ivan Rakitic, Marcelo Brozovic, Ante Rebic, Luka Modric, Ivan Perisic; Mario Mandzukic

Muhimu:-

Hadi sasa, mabao 151 yamefungwa katika kombe hili la dunia katika mechi 58.   Hii ikiwa na maana kuwa angalau kila mechi mabao mawili yamefungwa.

Kwa mara ya kwanza, kuna mabao mengi ya kujifunga anbayo ni 11. Mara ya mwisho, hali hii kushuhudiwa ilikuwa ni mwaka 1998, wakati kulikuwa na mabao 6 ya kujifunga.