rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Kombe la Dunia Urusi 2018 Senegal Colombia

Imechapishwa • Imehaririwa

Senegal inahitaji sare au ushindi kufuzu hatua ya mwondoano

media
Wachezaji wa timu ya taifa ya Senegal wakishangilia bao dhidi ya Japan wiki iliyopita REUTERS/Marcos Brindicci

Timu ya taifa ya soka ya Senegal ina kibarua kizito dhidi ya Colombia katika mchuano wake wa mwisho wa kundi H, AlhamisiĀ  jioni kuanzia saa 11 saa za Afrika Mashariki.


Mechi hii ni muhimu kwa Teranga Lions ambayo inahitaji sare au ushindi ili kufuzu katika hatua ya robo fainali.

Senegal inakwenda katika mchuano huu ikiwa na alama nne, baada ya ushindi wa mechi moja na kutoka sare katika mchuano huo.

Colombia nayo ina alama tatu, baada ya kushinda mechi moja na kupoteza mwingine.

Mara ya mwisho kwa timu hizi mbili kukutana ilikuwa ni mwaka 2014 wakati wa mchuano wa Kimataifa wa kirafiki na kutoka sare ya mabao 2-2.

Mwaka 2002, wakati wa kombe la dunia, timu hizi mbili zilikutana katika mchuano wao wa mwisho na kutoka sare ya 3-3.

Ratiba ya mechi nyingine:-

Japan vs Poland

Uingereza vs Ubelgiji

Panama vs Tunisia

Tayari Tunisia, imeondolewa katika michuano hii baada ya kupoteza michuano yake miwili, dhidi ya Ubelgiji na Uingereza.