rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Simba SC Kenya

Imechapishwa • Imehaririwa

Simba yakamilisha usajili wa Meddie Kagere kutoka Gor Mahia

media
Meddie Kagerea kushoto akisaini mkataba wa kuitumikia Simba Instagram/Shafii Dauda

Klabu ya Simba imefanikiwa kumsajili Gor Mahia ya Kenya, Meddie Kagere.


Ripoti kutoka Tanzania zilizomnukuu Meneja wa mchezaji huyo Patrick Gakumba akisema kwa asilimia kubwa kila kitu kimekamilika.

“Tumekubaliana na Simba, dili limekamilika, amesaini na kilichobaki ni Simba kumtangaza hadharani,”amesema Gakumba.

Gor Mahia imemsajili Erisa Ssekisambu ili kuziba nafasi ya Meddie Kagere.

Mchezaji huyo alifanya vyema kwenye michuano ya Sports Pesa na amekuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Gor Mahia ambacho kinashiriki hatua ya makundi ya taji la shirikisho Afrika.

Awali, ilitajwa mchezaji huyo alitajwa kuwaniwa na Yanga lakini Simba iliingilia kati.

Kagere ni mnyarwanda ambaye alizaliwa nchini Uganda.