rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Uganda

Imechapishwa • Imehaririwa

Mchezaji wa Uganda kujiunga na Gor Mahia

media
Mchezaji wa Uganda, Erissa Ssekisambu soks25east

Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Uganda, Erissa Ssekisambu amewasili nchini Kenya kukamilisha uhamisho wa kujiunga na Gor Mahia.


Mchezaji huyo amenukuliwa na vyombo vya habari nchini Uganda akisema hana mpango wa kusalia na mabingwa wa soka nchini humo, Vipers.

Usajili huo unakuja baada ya kocha wa Gor Mahia, Dylan Kerr kuarifu uongozi wa Gor Mahia kuwa timu hiyo inahitaji mshambuliaji mwingine atakayesaidiana na Jacques Tuyisenge na Meddie Kagere.

Ssekisambu alianza kuitumikia Uganda Cranes mwaka 2015 wakati huo ikinolewa na Mserbia, Sredojevic Milutin, Micho.