rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Kombe la Dunia Urusi 2018 Urusi Timu ya Taifa ya Nigeria Timu ya Taifa ya Croatia

Imechapishwa • Imehaririwa

Gernot Rohr:Tulifanya makosa mengi dhidi ya Croatia

media
Kocha wa Nigeria Gernot Rohr (kulia) akizungumza baada ya mchezo dhidi ya Croatia June 15, 2018 pembeni yake ni nahodha wa Nigeria, John Obi Mikel REUTERS/MATTHEW CHILDS

Siku moja baada ya timu ya Taifa ya Nigeria 'Super Eagles' kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Croatia katika fainali za Kombe la dunia zinazoendelea nchini Urusi, Kocha Mkuu wa Timu hiyo, Gernot Rohr amesema kikosi chake kilifanya makosa makubwa katika mchezo huo.

 


Rohr ametoa matamshio hayo baada ya Nigeria kushindwa kwa mabao 2-0 na Croatia, mabao yaliyofungwa kila kipindi na Oghenekaro Etebo aliyejifunga na bao la penati la kiungo Luka Modric. Mchezo baina ya timu hizo ulichezwa kwenye uwanja wa Kaliningrad Arena.

“Tunajua tulifanya makosa, makosa mengi muhimu na ni ukweli tunapaswa kuongeza ari na kuwa vizuri ili tusonhe mbele,”amesema Rohr na kusema kikosichake kinapaswa kuwa makini na kuzuia mipira ya adhabu kwa weledi.

Nahodha wa Nigeria 'Super Eagles' John Obi Mikel ameiambia RFI kwamba Nigeria inapaswa kuimarika ili kufanya vizuri kwenye mechi zilizosalia. Timu nyingine za Afrika zilizoanza vibaya kwenye michuano hiyo ni Misri ambayo ilipoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Uruguay na Morocco ambayo ilifungwa bao 1-0 na Iran.

Usikose kusikiliza makala ya Jukwaa la Michezo katika matangazo yetu ya jioni ili kupanda undani kuhusu mwanzo mbaya wa timu za Afrika kwenye fainali za Kombe la dunia.