rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Yanga SC Simba SC Tanzania

Imechapishwa • Imehaririwa

Azam yamsajili beki wa Timu ya Taifa ya Uganda

media
Beki wa kimataifa wa Uganda, Nicholaus Wadada (kushoto)akisaini mkataba wa kuitumikia Azam Mwanaspoti

Klabu ya Azam imeendelea kuimarisha kikosi chake baada ya kumsajili beki wa kimataifa wa Uganda, Nicholaus Wadada.


Wadada mlinzi wa pembeni amesajiliwa kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea klabu ya Vipers ya Uganda.

Kabla ya kusajiliwa na Azam, Wadada pia alikuwa akitajwa kuwaniwa na Simba na Yanga.

Anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na Kocha mpya wa Azam, Hans Pluijm. Wengine waliosajiliwa ni Tafadzwa Kutinyu, Donald Ngoma na Ditramu Nchimbi.

Aidha klabu hiyo imefanikiwa kumrejesha kundi mchezaji Mudathir Yahya ambaye msimu uliopita aliitumikia Singida United.