rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Simba SC Tanzania

Imechapishwa • Imehaririwa

Simba yavuna tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara

media
Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi ni mmoja ya wachezaji watatu wa klabu hiyo walioteuliwa kuwania tuzo ya mchezaji borta wa Ligi Kuu GOAL.COM

Klabu ya Simba imefanikiwa kupata tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa mwaka 2017/18 baada ya wachezaji wake watatu kuorodheshwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa Ligi hiyo.


Wachezaji Erasto Nyoni, John Bocco na Mganda Emanuel Okwi watawania tuzo hiyo katika hafla itakayofanyika Juni 23 mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Nyoni, Bocco na Okwi wamepita katika mchujo ambao awali ulikuwa na wachezaji 30 kutoka klabu mbalimbali.Wachezaji hao walikuwa msaada kwa Simba ulioiwezesha kumaliza ukame wa miaka mitano wa kutoshinda taji la Ligi Kuu.

Majina ya wachezaji hao yamepitishwa na kamati ya tuzo ambapo manahodha wa timu zilizoshiriki ligi hiyo msimu uliopita sambamba na wahariri wa michezo watapiga kura kumchagua mshindi.

Mbali na tuzo ya mchezaji bora, tuzo nyingine 15 zitatolewa katika hafla hiyo zikiwemo mchezaji bora chini ya miaka 20, timu yenye nidhamu, mwamuzi bora, mwamuzi bora msaidizi, kipa bora, kocha bora na goli bora.

Nyingine ni mchezaji wa heshima na kikosi bora kitakachotangazwa siku ya shrehe hizo.