rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Urusi Saudi Arabia Kombe la Dunia Urusi 2018

Imechapishwa • Imehaririwa

Kombe la Dunia 2018: Mashabiki wafurika Moscow

media
Mashabiki kutoka bara la Amerika wakiendelea na kusherehekea ufunguzi wa michuano ya Kombe la Dunia karibu na ikulu ya Kremlin. Moscow, Juni 13, 2018. Vasily MAXIMOV / AFP

Ndani ya saa chache zijazo,michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 itakua imeanza nchini Urusi. Sherehe za ufunguzi wa michunao hiyo zimefanyika katika uwanja wa Luzhniki, mjini Moscow.


Mechi ya ufunguzi itawahusisha wenyeji Urusi dhidi ya Saudi Arabia, na makumi ya maelfu ya mashabiki kutoka kote ulimwenguni wameendelea kuelekea kwa wingi katikati ya mji mkuu wa nchi hiyo, Moscow.

Mechi kati ya Urusi na Saudi Arabia itaanza saa kumi na mbili jioni saa za Afrika Mashariki.

"My name is Mark and Icame here from Australia. I'm here for the World Cup! Anaitwa Mark, ana umri wa miaka 60 na amewasili Moscow, tayari kwa mchezo wa Jumamosi dhidi ya Les Bleus ya Didier Deschamps.

"Oh, ilikuwa safari ndefu," amesema. Ilituchukua siku moja na nusu ili kufika hapa. Unajua, Australia ni mbali na hapa, lakini inatokea mara moja tu katika maisha. Hasa ikiwa tutaweza kuishinda Ufaransa! "

Michuano hiyo itashirikisha nchi 32, wakiwemo mabingwa watetezi Ujerumani, na itakuwa na mechi 64 zitakazochezwa katika kipindi cha siku 32.

Michuano hiyo ya mwezi mmoja inatarajiwa kuwavutia mashabiki nusu milioni kwenda Urusi na kote duniani inatarajiwa kutazamwa na watu zaidi ya bilioni tatu.

Kuna makundi manane, kila kundi likiwa na timu nne.

Timu mbili ambazo zitamaliza juu kwenye kundi ndizo zitakazosonga hadi hatua ya 16 bora.

Kwa upande wa fainali za sasa za Kombe la Dunia ambazo ni za 21 zitachezwa katika viwanja 12 katika miji 11 nchini Urusi, ambayo inapatikana eneo la upana wa maili zaidi 1,800.