Pata taarifa kuu
FIFA-MOROCCO-URUSI-SOKA

Kombe la Dunia 2026: Morocco yapoteza dhidi ya Amerika Kaskazini

Shirikisho la Kabumbu Duniani (FIFA) limetangaza kwamba nchi za Marekani, Canada na Mexico kwa pamoja zimeshinda dhidi ya Morocco katika kura iliyopigwa kuchagua nchi ambayo itakuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2026.

Nembo ya Shirikisho la Soka Duniani FIFA.
Nembo ya Shirikisho la Soka Duniani FIFA. REUTERS/Arnd Wiegmann/Files
Matangazo ya kibiashara

Zoezi hilo limefanyika katika mji mkuu wa Urusi, Moscow, wakati wa kikao cha 68 cha kongamano la FIFA.

Ushindani ulikiwa kati ya nchi ya Morocco inayoungwa mkono na nchi za Afrika na nchi 3 za Amerika Kaskazini zinazoungwa mkono na nchi za Ulaya.

Wajumbe kutoka nchi wanachama 207 walitumia kura yao kuamua Marekani, Canada na Mexico kuwa mwenyeji wa fainali za mwaka 2026.

Nchi za Marekani, Canada na Mexico kwa pamoja zinlionekana kuongoza katika uwezekano wa kushinda zabuni hii kutokana na miundo mbinu mizuri na usafiri wa uhakika.

Hata hivyo zabuni ya Morocco ilionekana kuwa kwenye makaratasi zaidi huku viwanja vingi vikiwa havijajengwa na wengi wanahoji ni namna gani nchi hiyo itaweza kwenda na kasi ya fainali za mwaka huo ambapo timu zitakuwa 48 kutoka 32 za sasa.

Marekani ilipoteza kwa Qatar itakayoandaa fainali za mwaka 2022, hatua iliyosababisha kubadilishwa kwa sheria za upigaji kura, ambapo awali wajumbe 24 wa kamati ya utendaji walikuwa wanaamua nani ataandaa, lakini safari hii wajumbe wote wa FIFA wamepiga kura kupata mshindi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.