Pata taarifa kuu
NIGERIA-DRC-SOKA-MICHEZO

Sintofahamu yaibuka katika timu ya taifa ya soka ya Nigeria

Wakati kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria kikitarajiwa kutupa karata yake ya kwanza ya michuano ya kombe la dunia nchini Urusi Jumamosi ya wiki hii dhidi ya Croatia, tayari kumeibuka hofu ya kutokea mgomo baridi kama ulivyoshuhudiwa wakati wa fainali za mwaka 2014 nchini Brazil.

Kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria, Super Eagles.
Kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria, Super Eagles. Reuters/Peter Cziborra
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo viongozi wa shirikisho la soka la Nigeria wanasema hawatarajii kuona tukio la mwaka 2014 likijirudia na kwamba tayari wamekubaliana na wachezaji wa kikosi hicho kuhusu malipo watakayopewa wakati wa fainali za mwaka huu.

Akizungumza na kituo kimoja cha kimataifa cha Al Jazeera, makamu wa rais wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Nigeria NFF, Shehu Dikko, mesema wanatarajia kuona wachezaji wakiitumikia nchi yao kuliko kudai malipo.

Haya yanajiri wakati huu zikiwa zimesalia siku nne tu kabla ya kuanza kutimua vumbi kwa fainali hizo nchini Urusi huku bara la Afrika likiwakilishwa na nchi za Senegal, Tunisia, Morocco, Misri na Nigeria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.