rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Kenya Tanzania Simba SC

Imechapishwa • Imehaririwa

Gor Mahia kumenyana na Simba FC Jumapili

media
Klabu ya Kenya ya Gor Mahia. Twitter. com/ Gor Mahia

Klabu ya Gor Mahia ya Kenya itamenyana na Simba FC ya Tanzania katika fainali ya kuwania taji la SportPesa, siku ya Jumapili.


Gor Mahia ambayo ni mabingwa watetezi, walufuzu katika hatua hiyo baada ya kuishinda Singinda United ya Tanzania mabao 2-0, yaliyofungwa na mshambuliaji Meddie Kagere, katika uwanja wa Afraha mjini Nakuru.

Mchuano mwingine wa awali, Simba FC iliishinda Kakamega Home Boys kwa mabao 5-4 kupitia mikwaju ya penalti, baada ya mchuano huo kumalizika kwa kutofungana.

Mshindi kati ya Gor Mahia na Simba FC, atamenyana na klabu ya Uingereza Everton katika mchuano wa kimataifa wa kirafiki katika uwanja wa Goodison Park mwezi ujao, lakini pia atapata kombe la Dola elfu 30,000