rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Argentina Israeli Kombe la Dunia Urusi 2018

Imechapishwa • Imehaririwa

Mechi ya maandalizi kati ya Argentina na Israel yafutwa

media
Timu ya taiaf ya soka ya Argentina wakati wa mazoezi mjini Barcelona. REUTERS/Albert Gea

Argentina imefuta mechi yake ya mwisho ya maandalizi ya Kombe la Dunia dhidi ya Israel mjini Jerusalem, mechi ambayo ingelipigwa Jumamosi wiki hii, mshambuliaji wa timu ya taifa ya soka ya Argentina, Gonzalo Higuain amesema.


"Kwa kweli wamechukua uamuzi mzuri," Bw Higuain amesema katika mahojiano na kitiuo cha ESPN, akithibitisha taarifa zinazosema kwambamechi hiyo imefutwa kutokana na shinikizo la kisiasa.

Mechi dhidi ya Israeli imezua ukosoaji mkubwa kutoka kwa rais wa Shirikisho la Soka nchini Palestina, ambaye wiki iliyopita aliwataka mashambiki wa soka nchini humo kuchoma moto picha na nguo zenye picha ya mchezaji wa Argentina Lionel Messi kama atakubali kushiriki katika mechi hiyo.

Katika barua aliomwandikia mwenzake wa Argentina, Claudio Tapia, Rais wa Shirikisho la Soka nchini Palestina, Jibril Rajoub, aliishtumu wiki iliyopita Israel kutumia mechi hiyo kama "chombo cha kisiasa".

Mamlaka ya Israel ilichangia kifedha katika maandalizi ya mechi hiyo kuchezwa Jerusalem badala ya Haifa.

Raia wa Palestina wamekaribisha hatua ya kufutwa kwa mechi hiyo.

Huu ni "ushindi mkubwa na pigo kwa Israel", ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook mwanachama wa Kamati Kuu ya Vijana na Michezo nchini Palestina, Abdel-Salam Haniyeh.

Argentina itacheza mnamo Juni 16 mechi yake ya kwanza ya Kombe la Dunia, nchini Urusi.