Pata taarifa kuu
CAF-MICHUANO

Mataifa nane kushiriki michuano ya CAF mwishoni mwa mwaka 2018

Mechi za mzunguko wa mwisho kuwania nafasi kucheza fainali ya soka kwa mataifa ya Afrika kwa upande wa wanawake, inachezwa siku ya Jumatano.

Nigeria ndio mabingwa watetezi wa taji hili.
Nigeria ndio mabingwa watetezi wa taji hili. Reuters/Benoit Tessier
Matangazo ya kibiashara

Fainali ya mwaka huu, itakuwa ya 11 tangu kuanza kwa mashindano haya 1998 yanayoandaliwa na Shirikisho la soka barani Afrika CAF, kila baada ya miaka miwili.

Ghana itakuwa mwenyeji wa mashindano haya, yatakayokutanisha mataifa nane katika michuano itakayochezwa kati ya tarehe 17 Novemba na tarehe 1 mwezi Desemba.

Nigeria ndio mabingwa watetezi wa taji hili.

Mechi za kufuzu zitachezwa nyumbani na ugenini na mshindi, ataungana na wenyeji Ghana.

Ratiba:

Algeria vs Ethiopia

Cote d'Ivoire vs Mali

Gambia vs Nigeria

Congo vs Cameroon

Kenya vs Equitorial Guinea

Lesotho vs Afrika Kusini

Zambia vs Zimbabwe

Mechi za marudiano ni wiki ijayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.