Pata taarifa kuu
AFRIKA-KIKAPU-TANZANIA

Maandalizi ya kikapu chini ya miaka 18 kanda ya tano, yapamba moto Tanzania

Shirikisho la mpira wa kikapu tanzania TBF limesema maandalizi ya michuano ya kanda ya tano Afrika kwa vijana yanaendelea Jijini Dar es Salaam. Michuano hiyo inatazamiwa kufanyika Juni 17 hadi 22 mwaka huu.

Wchezaji wa mpira wa kikapu wakiwa uwanjani
Wchezaji wa mpira wa kikapu wakiwa uwanjani Mandatory Credit: Brad Rempel-USA TODAY Sports
Matangazo ya kibiashara

Tanzania itakuwa mwenyeji wa michuano hiyo ya vijana itakayoshirikisha mataifa 12 yanayounda kanda ya tano ya Afrika.Baadhi ya mataifa hayo ni Kenya, uganda, Ethiopia, Burundi, Misri na Sudan.

Rais wa Chama cha kikapu Tanzania, Fares Magesa ameiambia RFI Kiswahili kwamba katika kuelekea michuano hiyo TBF imepokea ahadi za michango kutoka kwa wadau mbalimbali.

“Tumepokea vifaa kutoka serikali kuu, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kampuni ya Siemens, na vyombo vya habari,” amesema Magesa, akizishukuru pia serikali ya Tanzania na serikali ya Mapinduzi ya Znzibar kwa kuendelea na jitihada za kufanikisha michuano hiyo.

Aidha katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Magesa amesema TBF inatazamia kupokea vifa vya misaada kutoka kwa wadau wa mpira wa kikapu waliopo nchini Marekani.

Katika michuano hiyo Tanzania, itawakilishwa na timu mbili, moja ya wanawake na nyingine ya wanaume.

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa michuano ya kikapu ya kanda ya tano Afrika kwa vijana chini ya miaka 18 kufanyika Tanzania.

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.