Pata taarifa kuu
BAISKELI-MICHEZO

Timu ya taifa ya Rwanda ya waendesha baskeli yaelekea Cameroon

Timu ya taifa ya Rwanda ya waendesha baskeli yaelekea Cameroon Timu ya Taifa ya Rwanda ya mchezo wa baiskeli imeondoka nchini humo kuelekea nchini Cameroon ambako itashiriki michuano ya baiskeli ya Tour Du Cameroon.

Jean Bosco Nsengimana mshindi wa Tour du Rwanda, Novemba 22, 2015 katika uwanja wa Amahoro, Kigali.
Jean Bosco Nsengimana mshindi wa Tour du Rwanda, Novemba 22, 2015 katika uwanja wa Amahoro, Kigali. Christophe Jousset
Matangazo ya kibiashara

Mashindano hayo ya kila mwaka yanatazamiwa kuanza Jumamosi wiki hii na yanatazamiwa kufikia tamati Juni 3 ambapo waendesha baiskeli wataendesha katika maeneo mbalimbali ya Cameroon.

Baadhi ya waendesha baiskeli waliokwenda nchini Cameroon ni pamoja na mshindi wa mbio za baiskeli za Tour Du Rwanda mwaka 2015, Jean Bosco Nsengimana, Bonaventure Uwizeyimana, Mshindi wa medali ya dhahabu katika michuano ya African games ya mwaka 2015 Janvier Hadi, mshindi wa mbio za baiskeli za Rwanda mwaka 2017 Patrick Byukusenge.

Wachezaji wengine chipukizi wanaounda kikosi cha Rwanda ni Didier Munyaneza na Jean Paul Kene Ukiniwabo.

Tangu mwaka 2010 waendesha baiskeli wa Rwanda wameshinda mara saba michuano ya baiskeli ya Tour Du Cameroon.

Nchi nyingine zinazotazamiwa kushiriki michuano hiyo ni Congo Brazaville, Gabo, Ivory Coast na wenyeji Cameroon.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.