Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-COSAFA-SOKA

Michuano ya Cosafa kuanza Jumapili

Michuano ya Cosafa inatazamiwa kuanza Jumapili nchini Afrika Kusini, huku waamuzi 18 wakiteuliwa kuchezesha michuano hiyo.

Mashindano ya Cosafa ya mwaka huu yatashirikisha timu 14 ambapo timu nane zitaanza hatua ya awali wakati timu nyingine nane zitaanzia hatua ya robo fainali.
Mashindano ya Cosafa ya mwaka huu yatashirikisha timu 14 ambapo timu nane zitaanza hatua ya awali wakati timu nyingine nane zitaanzia hatua ya robo fainali. REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Mashindano hayo yanafanyika nchini Afrika Kusini kwa mara ya tatu mfululizo, baada ya timu nyingine kutoonesha nia ya kuandaa michuano hiyo.

Mashindano ya mwaka huu yatashirikisha timu 14 ambapo timu nane zitaanza hatua ya awali wakati timu nyingine nane zitaanzia hatua ya robo fainali.

Baadhi ya timu zitakazoshiriki mashindano ya mwaka huu ni mabingwa watetezi Zimbabwe, Zambia, Namibia,Lesotho, Swaziland.

Timu nyingine ni Botswana, Madagascar, Angola, Ushelisheli,Msumbiji, Mauritius, Malawi na Comoro.

Afrika Kusini ilishinda taji hilo kwa mara ya mwisho mwaka 2016.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.