Pata taarifa kuu
FIFA-URUSI-KOMBE LA DUNIA 2018

Fahamu kundi G, kombe la dunia 2018

Kundi G:Hili ni kundi lenye mataifa yaliyo na vijana chipukizi wanaotaka kuonekana katika michuano ya kombe la dunia.Kundi hili lina Ubelgiji, Panama, Tunisia na Uingereza.Mechi ya kwanza ya kundi hili itakuwa kati ya Ubelgiji na Uingereza katika uwanja wa Kaliningrad.

Kundi la G fainali ya kombe la dunia
Kundi la G fainali ya kombe la dunia FIFA.COM
Matangazo ya kibiashara

Ubelgiji:

Timu ya taifa ya Ubelgiji
Timu ya taifa ya Ubelgiji FIFA.COM

Imewahi kucheza katika michuano ya kombe la dunia mara 12.

Fainali yake ya kwanza ilikuwa ni mwaka 1930.

Mara ya mwisho kushiriki ilikuwa ni mwaka 2014.

Imewahi kufika katika hatua ya nusu fainali mara moja. Mwaka 1986, Ubelgiji ilimaliza katika nafasi ya nne.

Kocha wa timu hii Roberto Martinez. Raia huyo wa Uhispania amewahi kuifunza Everton na Swansea.

Mchezaji wa kutegemewa katika kikosi hiki ni Eden Hazard. Ameifungia timu yake mabao sita katika michuano ya kufuzu na ana uwezo mkubwa wa kukimbia na kufunga mabao.

Panama

Timu ya taifa ya Panama
Timu ya taifa ya Panama FIFA.COM

Hii ndio mara ya kwanza, inashiriki katika fainali ya kombe la dunia, katika historia yake ya mchezo wa soka.

Kocha wa timu hii ni Hernan Dario Gomez raia wa Colombia, ambaye amekuwa akiifunza timu hiyo tangu mwaka 2014.

Jina lake la utani ni El Bolillo, na aliyewahi kuifunza nchi yake wakati wa fainali ya kombe la dunia mwaka 1998 na 2002.

Mchezaji wa kuangaliwa katika kikosi hiki ni Blas Perez ambaye amekuwa katika kampeni nne, za kufuzu katika kombe la dunia na kuifungia nchi yake mabao 11.

Tunisia

Timu ya taifa ya soka ya Tunisia
Timu ya taifa ya soka ya Tunisia FIFA.COM

Hii ni miongoni mwa mataifa ya Afrika yanayoshiriki katika fainali hii.

Haijawahi kushinda taji hili. Imeshiriki mara nne. Mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 1978, lakini mara ya mwisho ilikuwa ni mwaka 2006.

Imewahi pia kushiriki mwaka 1998 na 2002.

Miaka hiyo yote, Tunisia iliondolewa katika hatua ya makundi.

Kocha wa timu hii ni Nabil Maaloul, ambaye amewahi kuichezea timu yake ya taifa.

Miongoni mwa wachezaji wa kuangaliwa ni Issam Jemaa, ambaye ameendelea kuwa mfungaji bora wa timu hii.

Kikosi kilichotajwa na kocha Maaloul ni pamoja na:-

Makipa: Mathlouthi Aymen (Al Batin, Saudi Arabia), Ben Cherifia Moez (ES Tunis), Ben Mustapha Farouk (Al Shabab, Saudi Arabia), Moez Hassen (LB Chateauroux, Ufaransa )

Mabeki: Hamdi Nagguez (Zamalek, Misri), Dylan Bronn (Gent, Ubelgiji, Rami Bedoui (ES Setif), Yohan Ben Olouane (Leicester City, Uingereza), Siyam Ben Youssef (Kasimpasa, Uturuki, Yessine Meriah (CS Sfaxien), Bilel Mohsni (Dundee United, Scotland), Khalil Chammam (ES Tunis), Oussama Haddai (Dijon, Ufaransa ), Ali Maaloul (Al Ahly, Misri;

Viungo wa Kati: Elyess Skhiri (Montpellier, France), Mohamed Amine Ben Amor (Al Ahly, Saudi Arabia), Ghaylene Chalali (ES Tunis), Karim Laaribi (Cesena, Italia), Ferjani Sassi (Al Nassr, Saudi Arabia), Ahmed Khlil (Club Africain), Seifeddine Khaoui (Troyes, Ufaransa ), Mohamed Wael Arbi (Tours, Ufaransa );

Washambuliaji: Fakhreddine Ben Youssef (Al Ittifaq, Saudi Arabia), Anice Badri (ES Tunis), Bassem Srarfi (Nice, Ufaransa), Ahmed Akaichi (Al Ittihad, Saudi Arabia), Wahbi Khazri (Rennes, Ufaransa , Naim Sliti (Dijon, Ufaransa ), Sabeur Khlifa (Club Africain).

Uingereza:

Baadhi ya timu ya taifa ya Uingereza
Baadhi ya timu ya taifa ya Uingereza FIFA.COM

Imecheza katika fainali 14 zilizopita za kombe la dunia.

Ilishiriki katika fainali hiyo kwa mara ya kwanza mwaka 1950.

Mara ya mwisho kucheza katika michuano hii ilikuwa ni mwaka 2014.

Wamewahi kuwa mabingwa mara moja tu mwaka 1966.

Imecheza katika hatua ya nusu fainali mara mbili.

Kocha wa timu hii ni Gareth Southgate. Amekuwa katika nafasi hiyo tangu Septemba mwaka 2016.

Amewahi kuichezea timu yake inayofahamika kama Three Lions kama beki mwaka 1998 na 2002.

Mchezaji wa kuangalia katika kikosi hiki ni mshambulianaji Harry Kane ambaye aliichezea timu yake mara tano kuelekea katika michiuano hii.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.