rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Kombe la Dunia Urusi 2018 FIFA Timu ya Taifa ya Urusi

Imechapishwa • Imehaririwa

Fahamu kuhusu Uwanja wa Mordovia Arena, kuelekea fainali za Kombe la Dunia

media
Uwanja wa Mordovia Arena utakaotumiwa katika fainali za Kombe la Dunia nchini Urusi FIFA.COM

Uwanja huu unapatikana katikati ya Jiji la Saranski, Jiji dogo kabisa lenye wakazi 307000 litakaloandaa fainali za mwaka huu. Una uwezo wa kuchukua watazamaji 44,000 elfu kwa wakati mmoja.Klabu ya Mordovia itautumia uwnja huu baada ya kukamilika kwa fainali za Kombe la dunia.


Uwanja huu utaandaa mechi nne za hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Dunia ikiwemo mchezo baina ya Peru na Denmark utakaochezwa Juni 16.

Juni 19 Colombia na Japan zitachuana katika Uwanja huu, mchezo mwingine utakuwa baina ya Iran na Ureno utakaochezwa Juni 25 na mchezo wa mwsiho katika uwanja huu utachezwa Juni 28 baina ya Panama na Tunisia.