rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Tanzania Rwanda CAF

Imechapishwa • Imehaririwa

Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kuchezwa Jumatano hii

media
Kikosi cha wachezaji wa klabu ya Yanga FC. Issa Michuzi

Michezo kadhaa ya hatua ya makundi ya taji la Shirikisho Afrika inachezwa leo. Katika Kundi D Yanga ya Tanzania inaipokea Rayon Sports katika Uwanja wa Taifa mchuano ambao ni muhimu sana kwa Yanga

 


ikiwa inataka kusonga mbele katika hatua ya robo fainali.

Mchezo mwingine wa kundi hilo utakuwa baina ya Gor Mahia ya Kenya ambayo inaipokea USM Alger ya Algeria.

Mechi nyingine za taji la Shirikisho ni kama ifuatavyo:

Asec Mimosas itakuwa ugenini nchini Kongo kuchuana na AS Vita

Adouana Stars itachuana na Raja Casablanca

UD Songo na RS Berkane

Al Hilal na Al Masry

CARA Brazaville na Enyimba

Djoliba ya Mali itakumbana na Williumsville ya Ivory Coast