rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Timu ya Taifa ya Mexico FIFA

Imechapishwa • Imehaririwa

Mexico yataja kikosi cha awali, kombe la dunia

media
Kombe la dunia ambalo litakaloshindwa kuanzia mwezi juni hadi Julai nchini urusi FIFA.com

Kocha wa Timu ya Taifa ya Mexico Juan Carlos Osorio ametangaza kikosi cha awali cha wachezaji 28 watakaowakilisha nchi hiyo kwenye kombe la Dunia.


Katika kikosi hicho Osorio amemjumuisha mlinzi mwenye umri wa miaka 39 Rafael Marquez ambaye endapo atajumuishwa kwenye kikosi cha mwisho atakuwa anashiriki fainali za tano za Kombe la Dunia. Na ataakuwa sawa na wachezaji Gianluig Buffon, Lother Mattheus na Antonio Carvajal ambao pia wamecheza fainali tano za Kombe la Dunia.

Mexico imepangwa kundi F akatika michuano hiyo ikiwa na mabingwa watetezi Ujerumani, Sweeden na Korea Kusini.

Makipa Guillermo Ochoa (Standard Liege), Alfredo Talavera (Toluca), Jesus Corona (Cruz Azul)

Mabeki: Diego Reyes (FC Porto), Carlos Salcedo (Eintracht Frankfurt), Hector Moreno (Real Sociedad), Oswaldo Alanis (Getafe), Nestor Araujo (Santos Laguna), Miguel Layun (Sevilla), Jesus Gallardo (Pumas), Hugo Ayala (Tigres), Edson Alvarez (America)

Viungo: Hector Herrera (Porto), Andres Guardado (Real Betis), Rafa Marquez (Atlas), Jonathan dos Santos (LA Galaxy), Marco Fabian (Eintracht Frankfurt), Jesus Molina (Monterrey), Erick Gutierrez (Pachuca), Giovani dos Santos (LA Galaxy)

Washambuliaji: Javier Aquino (Tigres), Jesus "Tecatito" Corona (Porto), Raul Jimenez (Benfica), Oribe Peralta (Club America), Javier Hernandez (West Ham United), Carlos Vela (LAFC), Hirving Lozano (PSV Eindhoven), Jurgen Damm na Giovan Dos Santos ambaye anachezea LA Galaxy ya Marekani.

Timu nyingine zilizotaja vikosi vyake ni Brazil na Denmark.

Fainali za Kombe la Dunia zinatazmiwa kuanza Juni 14 hadi Julai 15.