Pata taarifa kuu
EVERTON-SAM ALLARDYCE-MARCO SILVA

Klabu ya Everton yamfuta kazi Kocha wake Sam Allardyce

Klabu ya Everton imetangaza kumfuta kazi Meneja wake Sam Allardyce ikiwa imepita miezi sita tangu alipochukua jukumu la kuinoa timu hiyo.

Kikosi cha Everton kilipowasili Dar es Salaam tanzania kwa ziara ya mechi za kirafiki mwaka 2017
Kikosi cha Everton kilipowasili Dar es Salaam tanzania kwa ziara ya mechi za kirafiki mwaka 2017
Matangazo ya kibiashara

 

Ripoti kutoka nchini Uingereza zinasema uamuzi huo umefikiwa ikiwa ni sehemu ya mikakati ya mmiliki wa timu hiyo .

Big Sam ameiongoza timu hiyo katika mechi 26 akishinda mechi 10 kutoka sare michezo saba na kufungwa mechi tisa, na ameiongoza timu hiyo kumaliza katika nafasi ya nane kutoka 13 alipoichukua katika Ligi Kuu ya England.

Inaelezwa Kocha wa zamani wa Hull City na Watford Marco Silva atachukuaa jukumu la kuinoa timu hiyo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.