rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Simba SC Yanga SC CAF Kombe la Shirikisho Afrika

Imechapishwa • Imehaririwa

Yanga kuchuana na Rayon Sports katika taji la Shirikisho Afrika

media
Nembo za mashindano ya CAF RFI Kiswahili

Timu ya Yanga SC ya Tanzania kesho Jumatano itashuika katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kuchuana na Rayon Sports katika mchezo wa hatua ya makundi wa taji la Shirikisho Afrika. Mchezo huo ni wa kundi D


Mechi hiyo itaanza saa moja kamili kwa saa za Afrika Mashariki ukiwa ni mchezo wa pili kwa kila timu ambapo Yanga ilishindwa kwa mabao 4-0 dhidi ya USM Alger wakati wapinzani wao Rayon Sports ilitosahana nguvu na Gor Mahia kwa sare ya bao 1-1.

Kocha Msaidizi wa Yanga Noel Mwandila amesema timu yake inaingia katika mchezo wa kesho dhidi ya Rayon Sports ikiwa na wachezaji wake mahiri Obrey Chirwa na Amis Tambwe.

Wachezaji hao wamekuwa nje kwa muda kutokana na majeraha.

“Chirwa na Tambwe wako fiti lakini pia Kamusoko, kuhusu Ajibu, nadhani bado hayuko sawasawa”amesema Mwandila.

Kocha huyo amesema hawatawadharau wapinzani wao kutokana na wao pia kuwa washindani katika muchuano hii.

Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub amesema timu yake haina cha kupoteza katika nchezo huo baada ya kufanya vibaya katika Ligi Kuu.

“Kila mchezaji analijua hilo. Mechi ya kesho ni ngumu na tunawaheshimu wapinzani wetu. Ushindi wa kesho utatupatia nguvu kama wachezaji na pia mashabiki wetu. Tunacheza nyumbani lazima tushinde.

Kocha wa Rayon Sports Ivan Minnaert amesema timu yake inaiheshimu Yanga na itaingia uwanjani kutafuta matokeo.

Yanga ilianza vibaya hatua ya makundi kwa kufungwa mabao 4-0 na USM Alger wakati wapinzani wao Rayon Sports walianza kwa sare ya bao 1-1 dhidi y Gor Mahia ya Kenya.

Mechi nyingine ya Kundi D itakuwa baina ya Gor Mahia na USM Alger.

Mechi nyingine za taji la Shirikisho ni kama ifuatavyo.

Asec Mimosas itakuwa ugenini nchini Kongo kuchuana na AS Vita

Adouana Stars itachuana na Raja Casablanca

UD Songo na RS Berkane

Al Hilal na Al Masry

CARA Brazaville na Enyimba

Djoliba ya Mali itakumbana na Williumsville ya Ivory Coast