rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Afrika Kusini Uhispania FC Barcelona

Imechapishwa • Imehaririwa

Mamelody Sundowns kumenyana na Barcelona Mei 16

media
Wachezaji wa Mamelodi Sundowns wakisherehekea ushindi wao. STRINGER / AFP

Uongozi wa klabu ya Mamelody Sundowns ya Afrika Kusini umethibitisha rasmi kuwepo kwa mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya mabingwa wa Uhispania Barcelona.


Mchezo huo utachezwa Mei 16 katika Uwanja wa FNB ikiowa ni sehemu ya maadhimisho ya kusherekea miaka 100 tangu kuzaliwa kwa rais wa kwanza wa taifa hilo, Nelson Mandela.

Hii itakuwa mara ya pili kwa klabu hizo kucheza nchini Afrika Kusini, mara ya kwanza ilikuwa 2007 ambapo Barcelona ilishinda mabao 2-1.

Awali chama cha soka nchini Afrika Kusini, SAFA kilibariki uwepo wa mchezo huo baada ya mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Jumanne.

Mbali na Mamelod, mchezo huo unaandaliwa pia kwa ushirikiano na Serikali ya Afrika Kusini, Mfuko wa Patrick Motsepe na Mfuko wa Nelson Mandela.