rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Burundi Afrika Judo

Imechapishwa • Imehaririwa

Mashindano ya bara Afrika kuwania taji la mchezo wa Judo Kuanza Burundi

media
Mashindano ya Judo yanafanyika Bujumbura. DR

Mashindano ya bara Afrika kuwania taji la mchezo wa Judo yataanza siku ya Alhamisi jijini Bujumbura nchini Burundi. Mashindano hayo yatazishirikisha nchi 13 kutoka Afrika.


Wachezaji 66 kutoka mataifa 12 wanatarajiwa kushiriki katika mashindano hayo makubwa kwa vijana barani Afrika.

Kati ya wachezaji hao, wachezaji 35 ambao wanafahamika kama Judoka, ni wanaume huku wanawake wakiwa ni 31.

Mataifa yanayoshiriki ni pamoja na Algeria, Djibouti, Misri, Gambia, Cote d'Ivoire, Madagascar, Morocco, Senegal, Afrika Kusini, Tunisia, Zambia na Zimbabwe.