rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Urusi FIFA

Imechapishwa • Imehaririwa

FIFA yalichukulia adhabu kali Shirikisho la soka la Urusi

media
Paul Pogba miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa (les Bleus). Reuters/Kai Pfaffenbach Livepic

Shirikisho la mchezo wa soka duniani FIFA, limeitoza faini ya Euro 25,000 Shirikisho la soka nchini Urusi kutokana na utovu wa nidhamu kwa mashabiki wa Urusi kutoa matamshi ya ubaguzi wa rangi dhidi ya wachezaji weusi wa Ufaransa.


Hatua hii inafuatia mashabiki wa Urusi kutoa matamshi ya ubaguzi wa rangi wakati wa chuano wa kimataifa wa kirafiki kati ya Ufaransa na wenyeji Urusi, mwezi Machi na Ufaransa kushinda kwa mabao 3-1.

Matamshi hayo yaliwalenga wachezaji weusi wa Ufaramsa Paul Pogba anayechezea Manchester United na Ousmane Dembele anayechezea pia klabu ya Barcelona.

Changamoto ya mashabiki wa soka nchini Urusi kutoa matamshi ya ubaguzi wa rangi imeendelea kuleta wasiwasi kuelekea fainali ya kombe la dunia mwezi ujao.

Na kwa sasa wachezaji weusi kutoka nchi za Ulaya na bara la Amerika wana wasiwasi mkubwa kukabiliwa na hali hiyo.

Haijafahamika kwamba Urusi itachukua hatua kali dhidi ya makundi ya watu hao wanaozagaza chuki kupitia ubaguzi wa rangi nchini humo katika michezo ya kimataifa au ya kirafiki na nchi za kigeni.