rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Morocco

Imechapishwa • Imehaririwa

Wanne wajeruhiwa katika shambulio dhidi ya basi la klabu ya Raja Casablanca

media
Klabu ya Morocco wakati wa mechi dhidi ya Uzbekistan, Machi 27, 2018 Casablanca. FADEL SENNA / AFP

Mashabiki wa klabu ya Raja Casablanca waliokua na hasira walishambulia kwa mawe basi liililokua limebeba wachezaji wa klabu hiyo. Tukio hilo lilitokea Jumatano usiku baada ya klabu hiyo kushindwa kufanya vizuri katika mchunao wake na klabu ya Rapide Oued Zem kutoka mji mdogo wa Oud Zem, kilomita 160 na Casablanca.


Katika mchuano huo Raja Casablanca ilisalimu amri kwa kufungwa mabao 3-1lao la kufutia machozi, na hivyo kushindwa kwa timu hiyo, kutwaa ubingwa.

Video zilizorushwa kwenye mitandao ya kijamii usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi wiki hii zinaonesha wachezaji, wakipigwa na mshangao, wakielezea shambulio hilo na kulaani kile kilichotokea. Mmoja wao amesema kwamba alitaka kufungua mashitaka dhidi ya wahalifu.

Wengine wamesema "walikua wamejitolea kwa Raja", wakiwakamashabiki kuwa wenye busara.

Msemaji wa Raja ameliambia shirika la habari la AFP kwamba watu wanne walijeruhiwa (wachezaji watatu na dereva), akiongeza kuwa klabu hiyo itafungua mashitaka.

Kocha wa Raja Casablanca, Juan Carlos Garrido, amekosoa mwenendo huo wa mashabiki akiwataka kuwa na upendo kwa wachezaji hata kama timu itakua imepoteza katika moja ya mechi.