Pata taarifa kuu
KENYA-RIADHA-IAAF

Mwanariadha wa Kenya ahusishwa na matumizi ya dawa za kuongeza nguvu mwilini

Bingwa mara tatu wa dunia katika mbio za 1,500 Asbel Kiprop, mwanariadha kutoka nchini Kenya, amekanusha madai kuwa amekuwa akitumia dawa zilizopigwa marufuku kumwongezea nguvu mwilini, kumsaidia kushinda mashindano mbalimbali ya Kimataifa, kwa mujibu wa ripoti zilizochapishwa katika vyombo vya Habari nchini Uingereza.

Mwanariadha wa Kenya Asbel Kiprop anayetuhumiwa kutumia dawa za kuongeza nguvu mwilini
Mwanariadha wa Kenya Asbel Kiprop anayetuhumiwa kutumia dawa za kuongeza nguvu mwilini PHOTO | AFP
Matangazo ya kibiashara

Kiprop mwenye umri wa miaka 28, ambaye alishinda medali ya dhahabu wakati wa michezo ya Olimpiki mwaka 2008, amesema hawezi kuharibu jina lake na kipaji chake kwa kutumia dawa hizo.

“Nimesoma ripoti ikinihusisha na matumizi ya dawa za kuongeza nguvu mwilini, mimi nimekuwa katika mstari wa mbele kupinga matumizi ya dawa hizo,” alisema Kiprop.

Shirikisho la riadha nchini Kenya AK kimesema kimesoma taarifa hizo lakini halikuwa na majibu kuhusu madai hayo.

Naye Wakala wa mwanariadha huyo raia wa Italia Federico Rosa amesema amesikia ripoti hiyo lakini hakuwa na maelezo ya kina.

Madai haya ya hivi punde ni pigo kwa taifa la Kenya lenya sifa kubwa katika mchezo wa riadha.

Wanariadha wengine ambao wamewahi kuhusishwa katika madai haya na baada ya kubainika kuwa kweli na kufungiwa na Shirikisho la riadha duniani IAAF ni pamoja na bingwa mara tatu wa mashindano ya Boston Marathon Rita Jeptoo na bingwa wa Olimpiki katika mbio za Marathon Jemima Sumgong.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.