rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

CAF CECAFA Burundi

Imechapishwa • Imehaririwa

Rais wa CAF kushuhudia fainali ya Cecafa kwa vijana, nchini Burundi

media
Le Malgache Ahmad. FADEL SENNA / AFP

Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika, CAF Ahamd Ahmad yu nchini Burundi ambapo kesho atahudhuria mchezo wa fainali za michuano ya taji la soka nchi za Afrika Mashariki na Kati kwa vijana chini ya miaka 17.


Mchezo wa fainali utazikutanisha timu za Tanzania na Somalia. ambazo ziliondoa Uganda na Kenya katika hatua ya nusu fainali.

Mashindano hayo yamedhaminiwa na shirikisho la kandanda duniani Fifa na Ripoti kutoka nchini Burundi zinasema maofisa wa Cecafa wamesifiwa kwa kuandaa kikamilifu michuano hiyo.

Katika hatua nyingine katibu Mkuu wa Cecafa Nicholaus Musonye amesema baada ya kukamilika kwa michuano hiyo, Cecafa itahamishia nguvu kuandaa michuano ya Cecafa kwa wanawake itakayofanyika mwezi ujao nchini Rwanda.

Hata hivyo michuano ya Cecafa kwa vijana chini ya miaka 17 inaelekea ukingoni lakini ilikumbwa na changamoto ambapo timu ya Taifa ya Vijana ya Zanzibar iliondolewa kwenye mashindano baada ya kubainika wachezaji wake kuzidi umri unaotakiwa.