Pata taarifa kuu
SOKA-SPORTPESA-UFADHILI-KENYA

SportPesa yarejea kufadhili soka nchini Kenya

Kampuni ya kubashiri mchezo SportPesa, imerejesha ufadhili wa ligi kuu ya soka nchini Kenya KPL.

Mkurugenzi wa SportPesa Ronald Karauri (Kushoto), Waziri wa Michezo Rashid Achesa (Katikati) na rais wa Shirikisho la soka FKF Nick Mwendwa (Kulia) wakiwahotubia wanahabari Aprili 23 2018
Mkurugenzi wa SportPesa Ronald Karauri (Kushoto), Waziri wa Michezo Rashid Achesa (Katikati) na rais wa Shirikisho la soka FKF Nick Mwendwa (Kulia) wakiwahotubia wanahabari Aprili 23 2018 twitter.com
Matangazo ya kibiashara

Mkurugenzi Mkuu wa SportPesa Ronald Karauri amesema kampuni yake itatoa Shilingi Milioni 685 kufadhili soka nchini humo kwa muda wa miaka mitatu ijayo.

Kati ya fedha hizo, Shirikisho la soka FKF, itapata Shilingi Milioni 69 huku ligi kuu KPL ikipangiwa Milioni 259.

Klabu ya Gor Mahia inayoshiriki michuano ya Shirikisho, itapokea Shilingi Milioni 198 huku AFC Leopards ikinufaika na Shilingi Milioni 159.

Hata hivyo, SportPesa haitaendelea na ufadhili wa michezo ya raga na bondia kama ambavyo ilikuwa inafanya hapo awali.

Mwaka uliopita, SportPesa ilijiondoa katika ufadhili wa michezo nchini humo baada ya serikali kuitaka kulipa kodi ya asilimia 35 kutoka kwa mapato inayokusanya kila mwaka.

Hii hatua kubwa kwa maendeleo ya mchezo wa soka nchini humo hasa kwa klabu ya Gor Mahia na AFC Leaoprds ambazo zina historia ndefu ya soka nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.