Pata taarifa kuu
JUMUIYA YA MADOLA-RIADHA-KENYA

Kenya yatawala mbio za Mita 3000 kuruka viunzi na maji

Kenya imeshinda mbio za Mita 3,000 kuvuka viunzi na maji kwa upande wa wanaume katika mashindano ya Jumuiya ya Madola inayoendelea nchini Australia.

Kutoka Kushoto: Mshindi wa medali ya Shaba Amos Kirui, mshindi wa medali ya dhahabu  Conseslus Kipruto na mshindi wa medali ya fedha  Abraham Kibiwott wakisherehekea baada ya kushinda mbio za Mita 3000 kuvuka viunzi na maji katika Uwanja wa Carrara katika
Kutoka Kushoto: Mshindi wa medali ya Shaba Amos Kirui, mshindi wa medali ya dhahabu Conseslus Kipruto na mshindi wa medali ya fedha Abraham Kibiwott wakisherehekea baada ya kushinda mbio za Mita 3000 kuvuka viunzi na maji katika Uwanja wa Carrara katika ADRIAN DENNIS | AFP
Matangazo ya kibiashara

Kihistoria, Kenya imekuwa ikitawala mbio hizi. Bingwa wa Olimpiki katika mbio hizi Conseslus Kipruto, aliwaongoza wenzake watatu kunyakua medali ya dhahabu, fedha na shaba.

Kipruto aliibuka mshindi kwa muda wa dakika 8 sekunde 10 nukta 08 akifuatwa na Abraham Kibiwott aliyemaliza kwa muda wa 8:10.62.

Medali ya shaba imemwendea Amos Kirui aliyemaliza kwa muda wa 8:12.62.

Baada ya ushindi huo, Kipruto amesema alitaka Wakenya wenzake kuchukua nafasi ya pili na ya tatu na hivyo aliendelea kuwahimiza.

“Sikutaka kuwaacha wenzangu nyuma, ili washindwe,” alisema.

“Niliwahimiza twende pamoja na nilipoona wamechoka, nikaamua kumalizia,” aliongeza.

Ushindi huu umeiongozea Kenya medali katika jedwali ikiwa na medali mbili za dhababu baada ya kushinda mbio za Mita 800 siku ya Alhamisi.

Matokeo kamili:-

1. Conseslus Kipruto (Kenya) 8:10.08

2. Abraham Kibiwott (Kenya) 8:10.62

3. Amos Kirui (Kenya) 8:12.62

4. Matthew Hughes (Canada) 8:12.33

5. Albert Chemutai (Uganda) 8:19.89 (PB)

6. Jonathan Hopkins (Wales) 8:34.12

7. Ieuan Thomas (Wales) 8:40.02

8. Adam Kirk-Smith (Ireland Kaskazini) 8:48.40

9. James Nipperess (Australia) 8:58.16

10. Simon Charley (Vanuatu) 10:03.08

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.